Kocha wa Algeria Vahid Halilhodzic amejiuzulu licha ya ombi la kibinafsi kutoka kwa rais Abdelaziz Bouteflika akimsihi asijiuzulu.
Vahid ambaye amekuwa Kocha wa timu ya Algeria kwa takriban miaka mitatu na hapo awali meneja wa timu ya Ivory Coast, alikataa ombi hilo akidai kuwa kuna changamoto za kimichuano.
Vahid ambaye ni mzaliwa wa nchi ya Bosnia alielekeza timu hiyo katika michuano ya kutoana. Timu yake ilikuwa imesalia kati ya timu zingine kumi na sita bora katika kitengo hicho cha ligi ya kombe la dunia.
Timu ya Algeria baada ya kuilaza South Korea mabao manne kwa mawili, haikuponea mchujo baada ya kulazwa mabao mawili kwa moja dhidi ya timu ya Ujerumani.
Hapo awali, katika michuano ya kufungua ligi ya kombe la dunia Algeria ililazwa mabao mawili kwa moja dhidi ya Belgium, na kutoka sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Urusi na kufuzu kwenda raundi ya pili
No comments:
Post a Comment