Thursday, 3 July 2014

KILA JAMBO NA WAKATI WAKE...

Picha hizo mbili zinamuonyesha mtoto huyo ambaye hakuweza kufahamika jina lake wala mama yake, akiwa ametolewa kwenye mfuko wa Salfet aliokuwa amehifadhiwa na kutupwa, hiyo khanga ni kutoka kwa msamaria mwema
Katika hali ya kutatanisha wananchi wa Soweto jijini Mbeya wamekutana na Kifurushi ambacho ndani yake kulikuwa na mtoto mchanga amewekwa na kutupwa akiwa amefariki, ikiwa ni tukio la pili kutokea eneo hilo baada ya tukio kama hilo kutokea wiki mbili zilizopita.


Na Mathias Canal
Wasomaji wetu,
Wapo wanaovamia shari japo mambo yanakuwa si shwari, wasichana wengi wa umri mdogo hususani wale ambao ni wanafunzi wa Sekondari wamekuwa wakivalia njuga mambo ambayo bado wakati wake.
Wanafunzi hawa ndio wanaosababisha wimbi kubwa la utupwaji watoto wachanga, nasema kila jambo na wakati wake kwa kuwa kama wakati ungekuwa umefika mabinti hwa wasingetoa mimba badala yake wangezaa.
Ongezeko la utupaji vichanga linazidi shamiri nchini Tanzania kutokana na wanawake wengi kukosa utu, na huruma hakika zipo sababu nyingi zinazosababisha wanawake kutupa watoto ikiwa ni pamoja na umri mdogo, na wanaume zao kuwatelekeza.
Hakika Kila jambo na wakati wake, kama wakati bado haujafika hakuna haja ya kuchumia kivulini na kulia juani wakati watu huchumia juani na kulia kivulini.
Ni neno la leo.
Team Kwanza Jamii/Mjengwablog-Iringa

1 comment:

Anonymous said...

aziz bilalI 06:03





hii ndiyo akheri zaman,astaghafirlullah ee mola tuepushe na mambo ka haya.

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!