Sunday, 13 July 2014

DESMOND TUTU AUNGA MKONO SHERIA YA KUJITOA UHAI


Aliyekuwa Askofu mkuu wa kanisa la kianglikana nchini Afrika kusini Desmond Tutu


Aliyekuwa Askofu mkuu wa kanisa la kianglikana nchini Afrika kusini Desmond Tutu ameingilia kati mjadala kuhusu kuwasaidia wanaotaka kujitoa uhai,akisema kuwa anaunga mkono haki ya wale wanaougua kupitia kiasi kuamua kujitoa uhai kwa heshima.
Amesema kuwa alihuzunishwa na vile rafikiye Nelson Mandela alivyoteseka siku za mwisho za maisha yake na kwamba ilikuwa fedheha na ukiukaji wa heshima kwa shujaa huyo.
Katika ripoti yake ilioandikwa katika gazeti moja la Uingereza la Observer ,kiongozi huyo wa dini aliyestaafu amesema kuwa sheria zinazowazuia watu kusaidiwa kujitoa uhai zinazua maswali mengi kuhusu hali ya maisha na kuhusu vile watu wanavyotumia fedha ili kuongeza kipindi cha maisha yao.
Matamshi yake yanajiri wakati ambapo bunge la Uingereza linaandaa kujadili mswada wa kusaidiwa kujitoa uhai baadaye wiki hii.

Bwana Tutu pia ametaka sheria za Afrika kusini kuangaziwa upya kuhusu kusaidiwa kujitoa uhai.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!