Wednesday, 4 June 2014

YALIYOJIRI KWENYE VIWANJA VYA LEADERS WAKATI WA KUAGA MWILI WA MAREHEMU GEORGE TYSON, WENGI WAZIMIA, VILIO NA MAJONZI VYATAWALA

Mwili wa Marehemu George Tyson Ukiwasili Viwanja vya Leaders Jijini Dsm kwaajili ya Kuagwa na hatimaye Kesho Kusafirishwa Kuelekea Nchini Kenya kwa Mazishi(Mazishi huko Kenya yatafanyika Tar 14/06/2014.

 Mwili Ukipelekwa eneo Rasmi la Kuagia Wananchi.Mwili Umeshawekwa eneo lililoandaliwa kwaajili ya Kuaga.
Msanii Monalisi Mke wa Kwanza wa Marehemu akiwa na Mtoto wake aliyezaa na Marehemu George Tyson.
Mkuu wa Mkoa wa DSM.
 
Simanzi na Vilio Vimetawala kwa hawa watu wa Karibu kabisa na Marehemu George TysonMke wa Marehemu George Tyson akipozwa na
Ndugu wa Marehemu.
 Mwenyekiti wa Bongo Movie Steve Nyerere akiteta Jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dms.
Sehemu ya Waombolezaji.
 Uimbaji Ukiendelea Kusifu na Kumtukuza Mungu.Eden THE Rocker akiwa na Familia ya TV 1 wakati wa Kuuaga Mwili wa Marehemu George.
Wanafamilia wa TV1 alikokuwa anafanya kazi Marehemu.Msanii Zola D KIng ambaye anafanya kazi TV1 kwenye Kipindi cha Boys Boys akijumuika kwenyee Msiba huu.

Bongo Movie Family
Mkuu wa Mkoa akuwasihi Wasanii nchini kuendeleza Umoja wao katika shida na Raha kama wanavyofanya sasa.Waombolezaji.
 Muwakilishi Kutoka Mwanza upande wa Filamu akitoa Rambirambi.Dj Choka akiweka Sawa Mashine yake kwaajili ya Kunasa Matukio.

Huyu anaitwa MWAIPOPO aliwakilisha Kutoa neno kwa Niaba ya Marafiki wote wa George Tyson,Hakika alishindwa Kuzungumza Kutokana na Uchungu alioupata kwa Kumpoteza Mtu Muhimu na wakaribu kama George.
 Kuna wakati Mboni alilia sana Na Kuhitaji Kupata Maji.

 Mtangazaji Joyce Kiria akitoa Neno kwaajili ya Marehemu,Ikumbukwe Marehemu George Tyson Mzaliwa wa Kenya ndiye alianza Kuongoza Kipindi cha WANAWAKE LIVE siku za awali.
Mkuu wa Mkoa akibadilishana Mawazo na Uncle Lundenga HashimBoss wa Michuzi Media Uncle Michuzi akibadilishana Mawazo na Asha Baraka
 Mkali wa Social Network Le Mutuz akiwa na Wakali wa Bongo Movie.Msanii Roma Mkatoriki pia ameshiriki Zoezi la Kuuga Mwili wa Mpendwa wetu George Tyson.Zola D King.Msanii TEA(Kulia) akibadilishana na Mawazo na MwenzakeMkubwa Ruge Mtahaba akibadilishana Mawazo na Hashim Lundenga.Mchungaji akiombea Safari ya Marehemu George Tyson,Pia ameombea Wasanii Kuamini kwa Mungu na sio Miungu katika Kipindi hiki Kigumu.Maombezi yakiendelea na Kuvunja Nguvu za Giza na Pepo la Vifo ndani ya Bongo Movie.Waombolezaji waktoa Sadaka Maalum kwaajili ya Kuchangia Malezi ya Watoto wa Marehemu.Steve Nyerere,Mwenyekiti wa Bongo Movie akizungumza na Wasanii pamoja na Waombolezaji wengine,Kubwa amesisitiza Kuamini Mungu tu,Kuamini Miungu ni Kupoteza Muda na hakusaidii Chochote Kile.
Hawa ni Baadhi ya Wasanii waliozaliwa Kisanaa Mikononi mwa Marehemu George Tyson.
 Msanii Elizabeth Michel akichat Kidogo wakati Shughuli ya Kuaga Mwili wa Marehemu Ikiendelea.
Mtoto wa Marehemu George Tyson aliyezaa na Monalisa akisoma Ujumbe kwaajili ya Baba Yake.Inauma Kumpoteza Mzazi.Chini ni Mke wa Marehemu aliyekuwa anaishi naye hadi Mauti Yanamkuta.
Meya Jerry Slaa akizungumza na Waomborezaji.

 Mwili wa Marehemu George Otieno Okumu .https://scontent-a-fra.xx.fbcdn.net/hphotos-xfp1/t1.0-9/10306550_726892774039463_4978938742271743019_n.jpgMboni akiaga Mwili wa Mpendwa wake George TysonMkubwa Ruge Mtahaba.Mtangazaji Maimatha Wa Jesse
Mtangazaji Jerry Muro akitoa Heshima za Mwisho.
Katibu wa Shirikisho la Mziki Braiton.
Mke wa Marehemu akibusu Mwili wa Mme wake aliyekwisha Lala Usingizi wa Milele Marehemu George Tyson.
 Joyce Kiria akimuaga George.
Mtoto wa Marehemu akimuaga Baba yake.
Monalisa aliyekuwa Mke wa Marehemu George akiaga Mwili wa Marehemu.
Kuna Watanzania wengine walishiwa Nguvu na Kuzimia kwasababu ya Majonzi ya Kumpoteza Marehemu George Tyson.
 Mwili Ukiondolewa Viwanja vya Leaders kwaajili ya Kupelekwa Uwanja wa Ndege na Kesho saa 4 Asubuhi utasafirishwa kwenda Nchini Kenya Nyumbani kwa akina George kwa Mazishi yanayotegemewa Kufanyika Tar.14/06/2014 na Tanzania Wawakilishi Watatu,MMoja ni Rais wa Bongo Movie Tanzania na Wajumbe wawili Kutoka Mboni Show.

Picha/Maelezo na Festo Sanga wa Habari Kwanza Media/Blog.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!