RAIS Jakaya Kikwete amesema kwa sasa Tanzania ina watu milioni 48 na ifikapo mwaka 2016, kutakuwa na watu milioni 50 kutokana na ongezeko la asilimia 2.7 la kila mwaka.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa chapisho la tatu la kidemografia, kijamii na kiuchumi, Rais Kikwete alisema kasi kubwa ya ongezeko la watu inafanya serikali kujiandaa na mikakati ya kukabiliana na ongezeko hilo, ikiwemo kuhakikisha mpango wa maendeleo wa miaka mitano ambapo nchi inafikia uchumi wa kati.
Alisema lengo la sensa ya watu na makazi ni kuisaidia serikali kupata ufumbuzi wa mambo mbalimbali ikiwemo kuangalia maisha ya Watanzania, kuongeza kutoa juhudi za kuwahudumia.
Alisema sensa hiyo itasaidia kuangalia maeneo mapya ya watu wanaohitaji huduma zaidi ili kuyapatia ufumbuzi, pamoja na kusaidia vizazi vijavyo kuifahamu Tanzania ya mwaka 2012.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dk. Albina Chuwa, alisema chapisho hilo limeonyesha kuwa theluthi moja ya kaya za Tanzania zinaongozwa na wanawake, huku kaya za mijini zikiongezeka kwa idadi ya watu kuliko kaya za vijijini.
Pia alisema chapisho hilo limeonyesha asilimia 58 ya watu wenye umri wa miaka 15 na zaidi wameoa na kuolewa au kuishi na wenza wao.
Alisema kwa upande wa Watanzania wanaoishi nje ya nchi ni asilimia moja, huku kiwango cha watu wanaojua kusoma na kuandika kikiwa asilimia 78 kwa watu wenye umri wa miaka 15 na kuendelea
TZ-DAIMA
No comments:
Post a Comment