KESI ya madai ya kujimilikisha ardhi kinyume na sheria inayowakabili maofisa watatu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imeahirishwa hadi Agosti 14, mwaka huu.
Jaji wa Mahakama ya Ardhi, Hamisa Kalombola, aliahirisha kesi hiyo jana kutokana na washitakiwa kutofika mahakamani.
“Kama hati ya kuitwa mahakamani ilipelekwa kwa Katibu Mkuu, yawezekana hakukuwa na mawasiliano mazuri baina yao… hivyo nashauri hati nyingine itakayopelekwa wapewe wao wenyewe na kusaini, ili tuweze kuendelea,” alisema Jaji Kalombola.
Wakili wa mlalamikaji, Fabian Payowela, alikubaliana na maelezo ya Jaji Kalombola na kudai atafuatilia kujua kama watuhumiwa hao wamepatiwa hati za kuitwa mahakamani na kuzisaini ili waweze kuudhuria mahakamani ili kesi hiyo iweze kuendelea.
Kesi hiyo ambayo ilifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Septemba 3, 2009 na Bomani na Kampuni ya Uwakili, na kusimamiwa na wakili Payowela, haijawahi kusikilizwa hadi sasa.
Washitakiwa hao ni Ramadhan Ufyole, Doroth Wanzia na Hans Msumo ambao ni wathamini wa ardhi/viwanja waandamizi kutoka wizara hiyo, wanatuhumiwa na Felix Tembo kujimilikisha viwanja vyake vitatu vilivyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam.
Tembo, katika kesi hiyo namba 117/ 2009 anadai Ufyole alijimilikisha kiwanja namba 83 “J”, Wanzia kiwanja “D” namba 2150 na Msemo kiwanja “D” namba 2152
TZ-DAIMA
No comments:
Post a Comment