Sunday, 8 June 2014

WAKIMBIZI WA KISOMALI WAPATA URAIA TANZANIA

SERIKALI imewapa uraia wa Tanzania wakimbizi wa Kisomali wenye asili ya Kibantu 1,514 waliokuwa wanaishi Chogo, Wilaya ya Handeni, Tanga.

Wakimbizi hao walikimbia nchi yao baada ya vita kutokea mwaka 1990 ambapo baadhi yao 3,000 walikimbilia nchini kwa kutambua kuwa ndipo mababu zao walikotoka, serikali iliwapokea na kuwahifadhi katika kambi ya Mkuyu iliyopo Tanga ambapo walipata msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR).
Akizungumza jana baada ya kuwapa vyeti vya uraia wakimbizi hao, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mathias Chikawe alisema wakimbizi hao walihamishwa na serikali mwaka 2003 kutoka kambi ya Mkuyu kwenda kwenye makazi ya Chogo ili wapatiwe mashamba kwa ajili ya kilimo.
“Nachukua nafasi hii kuwapongeza wote waliopewa uraia wa Tanzania, wajisikie kuwa wao ni raia huru sawa na watanzania wengine… hata hivyo nawasihi muwe waadilifu na watiifu kwa sheria zote za nchi yetu,” alisema Chikawe.
Hata hivyo, waziri huyo aliwataka wakimbizi 150 ambao hawakuomba uraia wa Tanzania kwa nia ya kurudi kwao Somalia hali ya amani itakapopatikana, kuendelea kutii sheria za nchi zinazotawala hifadhi ya ukimbizi nchini.
Mwakilishi Mkazi wa UNHCR, Joyce Mends-Cole katika hafla hiyo aliishukuru serikali ya Tanzania kwa kuwapa uraia wakimbizi hao na shirika lake litaendelea kutoa misaada kwa wakimbizi waliobaki

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!