Kila mtu hapa duniani ana nyota yake katika mlolongo wa nyota kumi na mbili, kila nyota ina kazi zake za kufanya ili ufanikiwe zaidi katika maisha kama ifuatavyo.
Nyota ya punda(Aries).
Kazi wanazotakiwa kuzifanya watu hawa ni jeshi, kazi za uokoaji, michezo, uuzaji, upasuaji, kufundisha(ualimu) na masuala ya fedha.
Nyota ya ng’ombe(Taurus).
Waliozaliwa tarehe 20 april- 20 may.
Wenyenye nyota ya ng’ombe wanashauriwa kufanya kazi za muziki, kazi za chakula, ujenzi, kazi za mashamba, uhasibu na sanaa.
Nyota ya mapacha(Gemini).
Waliozaliwa tarehe 21 may- 21 june.
Wenye nyota hii wanatakiwa kufanya kazi za utangazaji, uchapishaji, ualimu, ushari na biashara za kusafiri.
Nyota ya kaa(Cancer).
Waliozaliwa tarehe 22 june- 22 july.
Watu hawa wanatakiwa kujihusisha na kazi za madawa, kazi za baharini, upishi, kuhudumia watoto, kazi za benki, kazi za usimamizi na kazi za uandishi.
Nyota ya simba(Leo).
Waliozaliwa tarehe 23 july- 22 august
Wenye nyota hii wanatakiwa kufanya kazi za usimamizi, michezo, usonara, uanamitindo, kucheza sinema, kazi za vijana na ualimu.
Nyota ya mashuke(Virgo).
Waliozaliwa tarehe 23 august- 22 september.
Wenye nyota hii wanatakiwa kujishughulisha na uchapishaji, uongozi, elimu, afya, biashara na ukatibu mukhtasi.
Nyota ya mizani(libra).
Waliozaliwa tarehe 23 september – 23 october.
Watu wa mizani wanatakiwa kufanya kazi za uhusiano wa jamii, ushauri wa ndoa, biashara yasanaa, ushauri wa mambo ya urembo, uanasheria na uhakimu.
Nyota ya ng’e(scorpio).
Watu waliozaliwa tarehe 24 october- 21 december.
Watu wa nyota hii wana takiwa kujihusisha na madawa, kazi za upelelezi, wachunguzi, mafundi bomba, kazi za historia ya mabaki ya viumbe na ushauri wa kimapenzi.
Nyota ya mshale(Saggitarius).
waliozaliwa tarehe 22 november -21 december.
Watu wa nyota hii wanatakiwa kufanya kazi za kusafiri,sheria, uandishi, ualimu, dini, michezo, jeshi na uuzaji.
Nyota ya mbuzi(Capricon).
Waliozaliwa tarehe 22 december- 19 january.
Watu wa nyota ya mbuzi wanashauriwa kufanya kazi za uinjinia, uchoraji wa ramani za majumba, saveya , kazi za serikali, siasa na udaktari wa meno.
Nyota ya ndoo(Aquarius).
waliozaliwa tarehe 20 january- 18 february.
Watu wa nyota hii wanatakiwa kujihusisha na kazi za ufundi wa umeme, kompyuta, uchunguzi wa kisayansi, kazi za kijamii, unajimu na kazi za mazingira.
Nyota ya samaki(Pisces).
waliozaliwa tarehe 19 february- 20 march.
Watu wa nyota ya samaki wanatakiwa kujihusisha na kazi za unesi, muziki, dansi, uigizaji, askari wa majini, kazi za kidini, kupiga chapa na kazi za kutoa ushauri
No comments:
Post a Comment