WATANZANIA wametakiwa kutumia fursa zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na kujipatia akiba, mafao na mikopo sawa na watu walioajiriwa.
Rai hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam juzi na Ofisa Mwandamizi Kitengo cha Hiari (NSSF), Salim Kimaro, wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake wajasiriamali.
Kimaro alisema katika jitihada za kuhakikisha kila Mtanzania anafaidika na mfuko huo, shirika lao limepanua wigo kwa watu wote ili wanufaike na huduma zinazopatikana.
Alizitaja huduma hizo kuwa ni pensheni, mafao ya matibabu na uzazi kama ilivyo kwa watu walioajiriwa.
“Nchi yetu inakadiriwa kuwa na watu milioni 44, ambapo nguvu kazi ya watu wa umri kati ya miaka 15-60 ni milioni 22.7, kati yao milioni 1.2 tu ndio wanahudumiwa na NSSF, hii inamaanisha watu milioni 21.6 ndio walioko katika ajira binafsi na hawafikiwi na mfuko,” alisema
No comments:
Post a Comment