Monday 9 June 2014

TUITUMIE MITANDAO KIMAENDELEO

MABADILIKO ya sayansi na teknolojia kwa kiasi kikubwa yamechangia maendeleo kwenye mataifa mbalimbali hapa duniani, hasa kwa watu kufanya ugunduzi, kusaka taarifa au kutangaza bidhaa husika.

Kukua kwa teknolojia ya mawasiliano kumekifanya dunia iwe kijiji hivyo kurahisisha mwingiliano wa jamii tofauti tofauti kiuchumi, kibiashara, kiutadamuni, kisiasa na kwenye sekta mbalimbali kulingana na mahitaji ya wahusika.
Tanzania nayo iliingia katika mabadiliko hayo kwa kulegeza baadhi ya sera, sheria na taratibu zake ili kutoa fursa zaidi kwa watu kujifunza na kushirikiana na wenzao waliopo nchi ya nchi.
Tunaamini kuwa uamuzi huu ulikuwa sahihi kwakuwa Tanzania isingebadilisha mambo yake ingeachwa nyuma kiuchumi na kiteknolojia.
Licha ya dhamira hiyo njema ya serikali bado kumekuwa na changamoto kubwa kwa baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kwa kuwachafua wengine iwe kwa maneno au kwa picha.

Tunajua kila mtu ana uhuru na haki ya kufanya mambo yake bila kuingiliwa na mwingi hivyo tabia iliyoanza kujitokeza hivi sasa ya watu kuchafuana kutumia mitandao si jambo jema.
Tunaamini kuwa mitandao ya kijamii inalenga kupanua uelewa wa watumiaji wake pamoja na kubadilishana taarifa kulingana na mahitaji ya wahusika hivyo si jambo jema mitandao ikawa chanzo cha kufaraka.
Tayari tumeona baadhi ya watu kwa sababu wanazozijua wao wamekuwa wakitoa taarifa au picha za faragha za watu mbalimbali hususan wasanii, wafanyabiashara na wanasiasa.
Matumizi ya aina hii kwa kiasi kikubwa yanarudisha nyuma jitihada za kutafuta maendeleo na pia yanasababisha jamii kuishi kwa visasi, chuki na mifarakano.
Ni jambo la busara kila mtumiaji wa mitandao hiyo akaitumia fursa ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia kuongeza uelewa, kudumisha amani, upendo na mshikamano ndani ya jamii.
Sote ni mashahidi kuwa mitandao ya kompyuta imesaidia sekta ya afya, elimu, simu na nyinginezo kukua zaidi na kubadilisha taarifa au ujuzi kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Tunamini kuwa bila ya mitandao ya kijamii, taifa lingekuwa likisuasua kwenye maendeleo pamoja na kutumia gharama kubwa katika elimu, afya na miundombinu.
Rai yetu kwa Watanzania wote ni kuitumia mitandao ya kijamii kwa faida zaidi badala ya kuweka picha za ngono, matusi au vitendo vyovyote vinavyochangia kuvunja utu wa mtu
TZ-DAIMA

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!