Friday, 6 June 2014

MBARONI KWA KUBAKA BIBI WA MIAKA 90

MAHAKAMA ya Mkoa wa Tabora, imemhukumu mkazi wa Kijiji cha Mabama wilayani Uyui, Malando Charles (30), kifungo cha miaka 30 jela na kulipa fidia ya Sh 500,000, baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka bibi kizee wa umri wa miaka 90.


Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi, Bahati Chipeto, alisema ameridhika na ushahidi uliotolewa mbele yake bila shaka yoyote.
Alisema kitendo alichokifanya mshtakiwa, ni unyama kwa bibi kizee huyo, kimemsababishia maumivu makali na ni udhalilishaji mkubwa kwa wanawake.
Hakimu Bahati alisema hukumu hiyo ni fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo nchini kote, hasa wenye lengo la kudhalilisha na kubaka wanawake.
Alisema tabia kama hizo zimekuwa zikitokea mara kwa mara, na Mahakama haitafumbia macho vitendo vya udhalilishaji kuendelea, badala yake itatoa adhabu kali ili vitendo vya aina hiyo vikomeshwe.
Awali Wakili wa Serikali, Miraji Kajiru, alidai mahakamani hapo kuwa usiku wa Februari 3 mwaka huu, katika Kijiji cha Mabama wilayani Uyui mkoani Tabora, Charles alimbaka bibi huyo (jina limehifadhiwa) na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili huyo alimuomba Hakimu kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa huyo, kwani vijana wana nguvu lakini wamekuwa wakifanya vitendo vya ajabu kwa jamii

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!