RAIS Jakaya Kikwete amesema hana wasiwasi na hali ya mjadala mkali, uliotawala Bunge Maalumu la Katiba, kwa sababu ni muhimu kwa mjadala kuhusu Katiba mpya, ukawa wa kina ili kuweza kupata Katiba bora kwa Watanzania.
Aidha, amesema Katiba ya Tanzania haitapatikana kwa mikutano ya kisiasa nje ya Bunge Maalum la Katiba, bali ndani ya Bunge hilo, ambako ni dhahiri kuwa mjadala utatawaliwa na nguvu ya hoja na busara.
Rais Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, alitoa ufafanuzi huo jana wakati alipotoa Mhadhara kuhusu Usalama wa Taifa kwenye Chuo cha Taifa cha Ulinzi kilichopo Kunduchi, Dar es Salaam.
Wakati wa kipindi cha maswali na majibu, ofisa mmoja wa Jeshi la Kenya alimuuliza Rais Kikwete kama alikuwa na wasiwasi kuhusu mjadala, unaoendelea nchini kuhusu Katiba mpya unaweza kuvuruga usalama wa Tanzania.
Akijibu kwa kujiamini, Rais Kikwete alisema: “Sina wasiwasi hata kidogo kwa sababu hatukutarajia kuwa mjadala wa Bunge Maalumu la Katiba kuhusu jambo hili kubwa, ungekuwa rahisi.
“Yalipojitokeza maoni ya Tanzania kupata Katiba mpya, tuliunda Tume, na tume hiyo ikatoa ripoti yake ambayo ndiyo inajadiliwa katika Bunge Maalumu. Hatukutarajia kuwa mjadala kuhusu ripoti ungekuwa rahisi kwa wajumbe kutoa majibu ya ‘ndiyo’ ama ‘hapana.”
Aliongeza kusema: “Kinachoendelea ni jambo muhimu na la lazima…najua wakati mwingine majadiliano yalikuwa makali mno, lakini hili ni jambo zuri. Aina ya mfumo na muundo wa Serikali lilizusha mjadala mkali, lakini hayo ni matokeo ya hali halisi ya masuala yanayojadiliwa.”
“Ni imani yangu kuwa tutafikia mwisho. Mwisho upi, hilo ni suala la Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kuamua. Muhimu ni kwamba Katiba mpya inaweza kupatikana kutoka bungeni tu siyo kupitia mikutano ya hadhara nje ya Bunge. Huko hakuna Katiba huko kuna mikutano ya hadhara na siasa tu. Katiba itapatikana kwa mijadala na kwa nguvu ya hoja ndani ya Bunge letu.”
Mihadhara ya nje ya Bunge, ingawa hakuitaja, ni ile inayoendeshwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani na wafuasi wao, ambao ni wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba ambao kabla ya kuahirishwa kwa muda Bunge hilo mwishoni mwa Aprili ili kupisha Bunge la Bajeti linaloendelea na vikao vyake, walisusia Bunge.
Walisusa kwa kile walichodai kutotaka kuburuzwa na wenzao wa CCM, ambao ni wengi ndani ya Bunge hilo, linalotarajiwa kurejea tena kwa siku
HABARI LEO.
No comments:
Post a Comment