Furaha bab kubwa!: Wachezaji wa Brazil wakishangilia ushindi wao wa penati 3-2 dhidi ya Chile na kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali.
WENYEJI Brazil wamekuwa wa kwanza kufuzu hatua ya robo fainali ya kombe la dunia baada ya jana usiku kuifunga Chile kwa mikwaju 3-2 ya penati kufuatia sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za kawaida na dakika 30 za nyongeza.
Kutokana na matokeo hayo, baadhi ya wachambuzi wa soka wameanza kuwa na wasiwasi na mwendo wa Brazil na kushindwa kutambua watafika hatua gani.
Lakini sapoti kubwa wanayopata kutoka kwa mashabiki wao inaweza kuwa motisha kubwa kwao na wakajikaza hatua inayofuata.
Jibu ni rahisi, yawezekana wakafika fainali na kutwaa ubingwa wao wa sita wa kombe hilo , lakini ukweli unabaki palepale kuwa wanahitaji kukaza sana.
Chile walicheza mpira mzuri na kuwabana Brazil kwa kila namna mpaka waliposubiri hatua ya mikwaju ya penati.
Gonzalo Jara aliyecheza Nottingham Forest msimu uliopita ndiye alikosa penati ya tano na ya mwisho kwa Chile. Mkwaju wake uligonga mwamba na baada ya hapo Taifa zima la Brazil lilipuka kwa shangwe, nderemo na vifijo wakishangilia ushindi.
David Luiz akishangilia baada ya kufunga penati yake dhidi ya Chile
Majanga: Alexis Sanchez akiugulia maumivu baada ya kukosa penati yake.
Mashujaa wa Brazil , Julio Cesar na David Luiz wakikumbatiana kwa furaha baada ya kushinda
Neymar akijitahidi kuzuia hisia zake za machozi kwa kumkumbatia bosi wake Luiz Felipe Scolari
VIA-FULLSHANGWE BLOG
No comments:
Post a Comment