Monday 23 June 2014

BRAZIL: ALGERIA YAUA, UBELGIJI YA FUZU!

Algeria imeiangushia kipigo Korea Kusini baada ya kuichapa mabao 4-2 katika mechi ya Fainali za Kombe la Dunia iliyochezwa kwenye Uwanja wa Beira-Rio mjini Porto Alegre, Brazil.

Kwa ushindi huo, Algeria imefufua matumaini ya kutinga hatua ya 16 bora kama ikiifunga Russia katika mechi yake ya mwisho ya hatua ya makundi.
Katika mechi hiyo Algeria walipata bao la kwanza dakika ya 26 lililofungwa na Islam Slimani akiwa amezongwa na mabeki wa Korea Kusini, kabla ya dakika mbili baadaye Rafik Halliche kufunga bao la pili kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona.
Algeria ilipata bao la tatu dakika ya 38 ambalo lilifungwa na Abdelmoumene Djabou na hivyo kwenda mapumziko ikiongoza 3-0.
Kipindi cha pili, Korea Kusini walipata bao la kwanza dakika ya 50 ambalo lilifungwa na Son Heung-min, lakini Algeria waliongeza bao la nne dakika ya 62 ambalo lilifungwa na Yacine Brahimi baada ya kupata pasi safi ya Sofiane Feghouli.
Hata hivyo Korea Kusini walifanikiwa kupata bao la pili dakika ya 72 ambalo lilifungwa na Koo Ja-cheol.
Katika mechi iliyochezwa awali kwenye Uwanja wa Maracana mjini Rio de Janeiro, Ubelgiji ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Russia zikiwa zimesalia dakika mbili kabla ya mechi kumalizika na hivyo kutinga hatua ya 16 bora kwani katika mechi ya kwanza iliichapa Algeria 2-1.
Bao la ushindi la Ubelgiji lilifungwa na Divock Origi dakika ya 88 akiunganisha vema krosi safi ya Eden Hazard kutoka winga ya kushoto.
Hivi sasa Ubelgiji imebakiza mechi dhidi ya Korea Kusini, wakati Algeria imebakiza mechi dhidi ya Russia.
Leo, Jumatatu, Juni 23, 2014
Australia              v              Hispania (Saa 1:00 usiku)
Uholanzi              v              Chile       (Saa 1:00 usiku)
Cameroon           v              Brazil      (Saa 5:00 usiku)
Croatia                 v                Mexico  (Saa 5:00 usiku)

1 comment:

Anonymous said...


Emmanuel AmoseYesterday 18:35


1
Reply

hongera sana Algeria..

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!