Thursday 5 June 2014

208 WAFARIKI KWA UGONJWA WA EBOLA NCHINI GUINEA

Maafisa wa afya wakiwazika waathiriwa wa homa ya Ebola
Maafisa wa afya duniani wanaarifu kuwa watu wasiopungua 208 wameaga dunia kutokana na virusi vya Ebola nchini Guinea baada ya ugonjwa huo kusambaa kwa siku za hivi karibuni.


Angaa watu 21 waliaga dunia na visa vingine 37 vinavyohusiana na Ebola kuripotiwa kati ya tarehe 29 mwezi Mei na tarehe 1 mwezi Juni na kufikisha idadi ya visa hivyo kufikia 328 katika taifa hilo lililoko magharibi mwa Afrika.

Hadi sasa, hakuna dawa za kuzuia wala kutibu Ebola- moja kati ya virusi hatari sana duniani.Kati ya visa hivi, 193 vilithibitishwa kupitia vipimo vya maabara.
Zaidi ya nusu ya vifo vya hivi karibuni vilitokea kusini mwa eneo la Guekedou, mahali ambapo ugonjwa huo ulianzia.
Visa vitatu vimedhibitishwa na vingine 10 vinavyodhaniwa kuwa wa ugonjwa huo vimeripotiwa katika nchi Jirani ya Sierra Leone.
Mgonjwa wa Ebola akipokea matibabu
Inaaminika kuwa watu kumi wameaga dunia katika taifa hilo, huku wengine kumi wakifariki nchini Liberia.
Wanaotoa misaada ya matibabu wamesema kuwa sababu moja ya ongezeko la ugonjwa huo ni kuwa watu wanakataa kwenda hospitalini kutibiwa na badala yake kuwaendea waganga.
Homa hiyo ina uwezo ya kuuwa hadi asilimia 90 ya walioathiriwa na huambukizwa wakati maji maji ya mwili, kama vile damu, mkojo na jasho la mtu au mnyama aliyeambukizwa yanapogusana na ya mtu mwingine.
Hata hivyo, binadamu wana nafasi nzuri ya kupona iwapo ugonjwa huo utatambuliwa mapema na kupata matibabu.

Wataalamu kutoka shirika la afya ulimwenguni pamoja na madaktari wasio na mipaka wanaofanya kazi katika eneo hilo wanachunguzwa baada ya uwezekano wa kuathiriwa na Ebola.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!