Sunday, 11 May 2014

WAGONJWA WA DENGUE WATIBIWA BILA KUPIMWA

Madaktari wa hospitali za Serikali jijini Dar es Salaam, wameanza kuwatibu watu wenye dalili za homa ya dengue bila uthibitisho wa vipimo kutokana na uhaba wa vipimo vya homa hiyo tangu katikati ya wiki.
Akizungumza na gazeti hili jana, mmoja wa madaktari Hospitali ya Temeke, Dk Amon Sabasaba alisema wameendelea kupokea wagonjwa wa homa hiyo, lakini kutokana na kukosekana vipimo, wamelazimika kuwatibu kwa uzoefu wa dalili ya homa hiyo. “Tunafanya kazi bila vipimo, bado tunaendelea kupokea wagonjwa, tunachokifanya ni kuwahoji na kuwapima na kama hawatakuwa na malaria au homa ya matumbo, basi watakuwa na dalili za dengue,” alisema Dk Sabasaba.
Alisema madaktari wote hivi sasa wanawaangalia wagonjwa kwa ukaribu zaidi kuliko awali kutokana na mlipuko wa homa hiyo.
Alisema ugonjwa huo ni tishio kwa wafanyakazi wa hospitali kutokana na wengi kuugua kwa nyakati tofauti, ikiwamo muuguzi mmoja aliyeugua na kufariki dunia wiki mbili zilizopita.
“Mpaka sasa madaktari sita wameshaugua homa hii na mmuguzi mmoja amepoteza maisha,” alisema Dk Sabasaba bila kutaja jina la aliyepoteza maisha.
Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wagonjwa waliokutwa na homa hiyo ni wanafunzi wa Chuo cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHAS) na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana Jangwani.
Mmoja wa madaktari wa Hospitali ya Muhimbili, aliliambia gazeti hili kuwa aliwahudumia wagonjwa sita wa homa hiyo katika nyakati tofauti
MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!