AyoTV na millardayo.com Nairobi zimepata nafasi ya kuzungumza na msemaji wa Polisi nchini Kenya Gatiri Mboroki anaethibitisha kwamba ni kweli gari la Mbowe lilikamatwa tarehe 25 April 2014 ambapo gari hilo baada ya kuvuka mpaka kuingia Kenya likitokea Tanzania lilibadilishwa namba.
Anasema ‘kutokana na visa vya ugaidi nchini Kenya baada ya Wananchi kuona gari imebadilishwa namba na kupaki kwenye hoteli wakaripoti Polisi, Polisi walikwenda na kumkuta dereva peke yake aliewaambia kwamba kiongozi wa chama ambae ni Freeman mwenye gari amekwenda Nairobi kwa ndege, hiyo ilileta utata kidogo kwa kujiuliza amekwenda Nairobi kwa ndege iweje aache gari?’
Kwa kumalizia Gatiri Mboroki amesema hakuna aliefungwa wala gari hilo halijawahi kutumika kwenye visa vya ugaidi nchini Kenya na wala halikuzuiliwa isipokua sababu pekee ya gari hilo kupelekwa Polisi ni baada ya kuonekana likibadilishwa namba.
CRD: MILLARD AYO
No comments:
Post a Comment