JESHI la Polisi mkoa wa Singida limefanikiwa kumkamata dereva wa basi la Summry T.799 BET, Paul Njilo mkazi wa jijini Dar-es-salaam aliyegonga askari polisi wanne na wananchi 15 na kusababisha vifo vyao.
Ajali hilo ilitokea Aprili 28 saa 2.45 usiku katika babara kuu ya Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Utaho tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida,SACP,Geofrey Kamwela amesema kwa sasa wanaendelea na taratibu za kisheria na watakapomaliza pamoja na upelelezi,dereva Paul aftafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
Katika hatua nyingine, Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki kupitia tiketi ya CHADEMA,Tundu Lissu,ameahidi kutoa msaada wa kisheria kwa ndugu waliopoteza ndugu zao kwenye ajali ya basi la Summry.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Diwani wa kata ya Mungaa (CHADEMA) Mtheo Alex wakati akizungumza kwenye hafla ya sala maalum ya kuombea watu 14 wakazi wa kijiji cha Utaho waliogongwa na basi la Summry.
Amesema mbunge huyo anatafuta nafasi ili afike kijijini hapo kutoa pole kwa wafiwa na vile vile atashughulikia taratibu zote za fidia zitakazotokananabimwa ya basi hilo T.799 BET mali ya kampuni ya Summry.
“Taratibu za bima huwa si za kumalizika kwa muda mfupi,kawaida huwa za muda mrefu,kwa hiyo ndugu zanguni, kwa hili tuwe wavumilivu na tuendelee kuamini kwamba mwanasheria wetu Tundu,atalimudu”,amesema.
Wakati huo huo, Diwani wa kata ya Kituntu (CCM),Naftali Gwae alikanusha uvumi kuwa rais Jakaya Kikwete alituma rambai rambi zikiambatana na fedha.
“Rais wetu alituma salamau za rambi rambi na wala sio fedha.Kwa hiyo ndugu zangu niwasihi tu kwamba wakati huu mgumu unaoambatana na majonzi,mengi yatasemwa mengi lakini tuwe makini na kuyafanyia uchunguzi kwanza”,amesema.
Aidha,uvumi ulioenea kwamba Diwani wa CCM na Mtendaji wamechukua kutoka ofisi ya kijiji nyaraka za benki zinazodaiwa kuonyesha kuwa kijiji hicho kina akaunti yenye zaidi ya shilingi milioni mia moja,si za kwelei ni uongo mtupu.
Kwa mujibu wa Diwani Gwae baada ya sala hiyo,waathirika wa ajali hiyo kila moja amepewa shilingi 212,500 ikiwa ni rambarambi kwa kupoteza ndugu.
Fedha hizo ni kutoka fedha za ubani za shilingi 5 milioni zilizotolewa na mmiliki wa kampuni ya summry,shilingi laki moja mkuu wa mkoa wa Singida na shilingi 150,000 zilizotolewa na wakazi wa kijiji cha Minying
No comments:
Post a Comment