Wednesday, 30 April 2014
WANA MTWARA KUWAONA WEMA NA DIAMOND JUKWAA MOJA KWA MARA YA KWANZA!
Inawezekana uliwahi waona kwenye matamasha mbalimbali Wema Sepetu na Diamond wakiwa pamoja lakini hua inakua kama ‘Sapraiz’ ili pengine kuleta hamasa kwa mashabiki wao,sasa rasmi hii ni show ya kwanza ambayo itamueka Diamond Platnumz na Wema Sepetu kwenye jukwaa moja.
Wakazi wa Mtwara wamepata zali hili la kuona mastar hawa wakiwa wanaupeleka usiku wa Hills and Tie ambao umedhaminiwa na kampuni ya simu za mkononiya Vodacom,Meneja Masoko wa Vodacon Kelvin Twissa amesema huu utakua mkoa wa Kwanza na kama Mtwara watatoa sapoti wanategemea kuifanya iwe tour.
Hii ni namba maalum kwa ajili ya wateja wa vodacom kuweza kununua tiketi kupitia M pesa kwa simu zao za mkononi ambapo kwa yeyote atakaenunua atapata punguzo la asilimia 20 namba hiyo ni 0754 980 769.
Hizi ni picha za kwenye mkutano na waandishi wa habari mchana wa leo kwenye ofisi za Vodacom zilizopo Mlimani City.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment