Rapa mfanyabiashara ambaye kwa sasa yupo namba moja kwenye orodha ya wasanii wa hip hop matajiri zaidi duniani Puffy Daddy ametangaza kupitia twitter kuwa ni shabiki mkubwa wa timu ya kikapu ya New York Knicks ila pia ni mfanyabiashara na atajiwe bei ya timu ya Clippers atainunua. Hii ni baada ya boss aliyetoa maneno ya kibaguzi kupewa adhabu kubwa ya kutoisogelea timu wa NBA maishani inayoweza kusababisha auze timu hio.
Thamani ya Puff Daddy ni dola milioni 700 na ni karibu sana na kuwa The First Hiphop Bilionea.
Jarida la burudani linalochunguza utajiri wa mastaa na thamani ya vitu wanavyo miliki linasema thamani ya L.A Clippers ni dola milioni 575 ambzo P.Diddy anaweza kujipanga akazitoa
Wengine waliotangaza nia ya kuinunua timu hiyo ni pamoja na bondia Floyd Mayweather, rapa Rick Rozay, nyota wa zamani wa mchezo wa kikapu Magic Johnson, bondia Oscar De La Hoya na bilionea anayemiliki vyombo vya habari na makampuni ya kutengeneza sinema David Geffen.
CRD:blog ya wananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment