TAMASHA la Kanumba Day linatarajiwa kufanyika leo katika Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam na kupambwa na burudani mbalimbali.
Leo ni siku ya kuadhimisha kifo cha aliyekuwa msanii wa filamu hapa nchini, Steven Kanumba, aliyefariki Aprili 7, 2012 akiwa nyumbani kwake Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa Tamasha hilo, George Wakuganda, alisema kila kitu kimekamilika, ilikuwa ikisubiriwa siku tu ya tukio.
Wakuganda, aliwataja wasanii maarufu wa filamu nchini ambao watapamba siku hiyo kuwa ni Wema Sepetu, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Patcho Mwamba, Benny Kinyaiya, Aunt Ezekiel, Dude na wengineo.
Alisema siku hiyo itakuwa endelevu kila mwaka kwa kumkumbuka mpendwa wao, ambapo umeanzishwa mfuko wa siku hiyo maalumu ya kihistoria uitwao ‘Kanumba The Great Foundation’.
Wakuganda alizitaja burudani zitakazopamba usiku wa leo kuwa ni bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Jahazi Modern Taarab huku upande wa wasanii wa muziki kipya ni Snura Mushi ‘Mamaa Majanga’, TMK Family, Juma Nature, Afande Sele, Babu Ayoub, Tunda Man, Dogo Janja na Linah
No comments:
Post a Comment