WATANZANIA wanaoishi na wagonjwa wenye matatizo ya akili wametakiwa kuwafikisha hospitali mapema wagonjwa hao kutokana na ugonjwa huo kutibika.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Daktari Bingwa wa maradhi hayo, Frank Massao, ambaye alisema watu wengi wanapokuwa na mgonjwa wa akili, hushindwa kuwafikisha hospitalini mapema jambo ambalo si jema.
Dk. Massao alisema familia nyingi zinashindwa kuwafikisha wagonjwa hao hospitalini na kukimbilia kwa waganga wakienyeji kutokana na kuamini kuwa wamerogwa.
Alisema wengine hutumia imani za kidini kwa kumuombea mgonjwa wakiamini kuwa ugonjwa huo umesababishwa na mapepo au mashetani.
“Ombi langu kwa Watanzania watambue kuwa maradhi ya akili yapo, wataalamu wa tiba ya ugonjwa huu wapo, hospitali zipo na huduma zinapatikana,” alisema.
Alisema familia huwafikisha hospitalini wagonjwa hao baada ya kuona sehemu hizo zimeshindikana.
No comments:
Post a Comment