RAIS wa Gambia Yahya Jammeh (ﻳﺤﻴﻰ ﺟﺎﻣﻊ) amesema anataka kutekeleza mabadiliko ya sheria yatakayopelekea lugha rasmi ya nchi hiyo kubadilishwa kutoka Kiingereza hadi lugha asili. “Hatuamini tena kuwa ukitaka kuwa Serikalini
lazima uzungumze Kiingereza. Inafaa tuzungumze lugha yetu,” Rais Yahya Jammeh alisema hayo wakati wa kuapishwa kwa Jaji Mkuumpya nchini humo. Tangazo hilo lilitolewa miezi michache baada ya nchi hiyo kutangaza inajiondoa kutoka Jumuiya ya Madola, inayojumuisha mataifa 54 yaliyokuwa chini ya ukoloni wa Uingereza. Gambia ilisema “haitakuwa tena mwanachama wa taasisi ya ukoloni mamboleo”. Uingereza ilionya hivi majuzi kuhusu pingamizi la rais huyo dhidiya Uingereza, ambaye mwaka jana alishutumu Uingereza na Amerika kwa kuandaa majaribio ya mapinguzi ya Serikali nchini humo.
Rais wa Gambia mwaka jana aliiambia dunia kupitia Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba tishio kubwa linalotishia
ustaarabu na utu wa mwanadamu ni kuwepo kwa kampeni na uhamasishaji wa Ushoga na usagaji. "Wale wote wanaokuza
ushoga ni kama wanataka kukomesha kuwepo kwa binadamu",aliuambia mkutano wa viongozi wa Dunia mjini New York kwa mujibu wa Gazeti la Huffington Post."Hili ni janga na sisi waislamu na waafrika tutapigana kumaliza tabia hii".Aliongeza kwa kusema,"Ulawiti katika namna yoyote ile ni uovu na ni kama kupambana na Mwenyezi Mungu. Hata kama italazimishwa kwa nguvu fulani kuwa ni haki kwa mwanadamu". "Gambia ni nchi ya waumini. Dhambi na matendo ya zinaa yapolakini Ushoga si wa kuvumiliwa katika nchi ya Gambia", aliongeza Rais Yahya Jammeh. Awali aliwaambia mashoga waondoke nchini Gambia au watakatwa vichwa. Mahusiano ya jinsia moja nchini Gambia ni haramu.Mwaka 2009 Jammeh aliwaambia maafisa wa jeshi waliopandishwa vyeo kwamba, hatutahamasisha usagaji na ushoga katika jeshi, Ni mwiko katika majeshiyetu,"Ntamfukuza mwanajeshi yoyote atakaye tuhumiwa kuwa Shoga au Msagaji katika Gambia. Sisi hatuna haja ya Mashoga katika majeshi yetu", alisema Rais huyo.
Rais wa Gambia Yahya Jammeh
No comments:
Post a Comment