Saturday, 29 March 2014

PINDA KUKUTANA NA `SURPRISE` LEO DODOMA

Stori: Ojuku Abraham


WAZIRI Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda leo atakutana na ‘surprise’ ya aina yake, wakati atakapokabidhi tuzo kwa mwanamke bora wa mwaka, ambaye hadi sasa bado hajafahamika ni nani kati ya wanawake wanne mahiri nchini, itakayofanyika katika Ukumbi wa The African Dream, Dodoma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ndiye atakuwa mgeni rasmi katika utoaji tuzo.
Wanawake hao ambao mmoja wao ataibuka kinara na kuondoka na Tuzo na zawadi maalum ni pamoja na Dk. Maria Kam, Dk. Asha Rose Migiro, Profesa Anna Tibaijuka na Mheshimiwa Anna Kilango Malecela ambao wamefikia hatua hiyo ya mwisho baada ya kuwashinda wenzao 150 walioanza kupigiwa nao kura.
Dk. Asha Rose Migiro.
Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, Meneja Mkuu wa Global Publishers iliyoratibu zoezi hilo, Abdallah Mrisho, waliamua kutoa tuzo hizo hasa baada ya kupata msukumo uliotokana na kuthamini michango ya wanawake nchini.
Alisema wadau hao walituma majina zaidi ya 30,000, lakini kamati iliyachuja kulingana na sifa za kila mmoja na kupata wanawake 150 ambao walianza kupigiwa kura kwa awamu. Awamu ya kwanza iliyochukua miezi miwili, iliwapata wanawake 20, iliyofuata iliwapata watano na ya mwisho iliwapata washindi hao wanne.
Prof. Anna Tibaijuka.
Mrisho alisema hafla hiyo itawahusisha waalikwa pekee ambao aliwataja kuwa ni pamoja na waheshimiwa wabunge wa bunge maalum la Katiba, wanaharakati na wawakilishi wa taasisi mbalimbali walioko mjini Dodoma kwa sasa.
Dk. Maria Kamm.
“Ikumbukwe kwamba washiriki hawa wote ni washindi, kila mmoja atapata tuzo, isipokuwa ile ya mshindi kidogo itakuwa tofauti na nyingine na zaidi, yeye atapata na zawadi nyingine,” alisema
Mh. Anne Kilango Malechela.
Mrisho alisema baada ya kutolewa kwa tuzo hizo mwaka huu, mara moja wataanza mchakato wa kumpata mwanamke mwingine kwa mwaka ujao.
Aidha, katika upande wa burudani, Mrisho alisema atakuwepo msanii anayepiga nyimbo za Kiafrika, Zaid na wasanii wengine wa Bongo Fleva.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!