Wizara ya Kilimo na Uvuvi Zanzibar meishukuru Serikali ya Japani kwa kuwamuwa kuwajengea Soko la kisasa kwa lengo la kuimarisha na kuleta maendeleo hapa Zanzibar
Mkataba huo umetiwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilmo na Uvuvi Dr. Kassim Gharibu pamoja na Manager of Fisheries Engeneris Company Of Japan , Tadashi Ogawa huko Ofisini kwake Maruhubi Mjini Zanzibar ikiwa ni njia moja ya kulete ushirikiano.
Amesema huu ni wakati muafaka kwa kujitokeza kwa Meneja huyo kutokana na kutokuwepo kwa soko la uhakika ambalo litakaloweza kuhifadhi samaki wengi wanaovuliwa hapa Zanzibar.
Aidha Dr. Kassim amesema hii ni njia ya kuiimarisha Serikali na kuwaletea maendeleo Wavuvi katika ufanyaji wakazi zao hasa kwa kipindi kigumu walichonacho.
Hata hivyo amesema kuwa faraja hiyo haitowanufaisha wavuvi tu bali na Wananchi kwa ujumla hasa wakati wanapohitaji Kitoweleo cha haraka katika Mji wao wa Zanzibar.
Vilvile amesema hadi hivi sasa bado hajapatikana Mkandarasi atakaeweza kusimsmia soko hilo lakini endapo ikiwa tayari itatangazwa tenda na kuweza kupatikana kwa haraka.
Amewashauri wananchi wanaolitumia soko hilo kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu na kwa lengo la kuwaletea faraja soko hilo.
Dr. Kassim Gharib amesema katika ujenzi wa Soko hilo litagharimu Sh. Bilion 14 hadi kumaliza kwake.bado haja patikana lakini
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment