MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), Eliezer Feleshi, amemfungulia shtaka jipya la kuua kwa kukusudia, mmiliki wa jengo la Ghorofa 16 lilioanguka Mtaa wa Indira Ghandi Jijini Dar es Salaam na kusababisha maafa ya watu (27) waliosadikiwa kufukiwa na kifusi cha ghorofa hilo Machi 28, mwaka jana.
Feleshi ameithibitishia FikraPevu kuwa washtakiwa hao wamefunguliwa shtaka jipya leo Jumatano Machi 12, mwaka huu, Katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu la kuua kwa kukusudia.
“Ninachojua ni kuwa kesi hiyo inaondolewa na kuwa substated with another kesi, kwa hiyo mashtaka ya awali yameondolewa yameunganishwa na mashtaka mapya ya mauaji ya kuua kwa kukusudia, tunasubiri kukamilika kwa upelelezi” alisema Feleshi.
Alisema hapo awali mshtakiwa huyo (Raza Hussein Raza) akiwa na wenzake alikuwa anakabiliwa na shtaka la kuua bila kukusudia lakini baada ya upande wa Serikali kugundua mambo mengine sasa mmiliki huyo atakabiliwa na Shtaka la kuua bila kukusudia.
Kwa mujibu wa Sheria za Nchi, kesi za mauaji haina dhamana kutokana na ukubwa wa tukio ambapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina uwezo wa kushughulikia kesi hiyo.
Kutokana na Sheria hiyo Hakimu wa Mahakama hiyo Devota Kisoka ameamuru watuhumiwa hao kupelekwa gerezani ili kusubiri Sheria kufuata mkondo wake, ambapo DPP anadaiwa kutofuata kipengele hicho.
Kutokana na Sheria hiyo Hakimu wa Mahakama hiyo Devota Kisoka ameamuru watuhumiwa hao kupelekwa gerezani ili kusubiri Sheria kufuata mkondo wake, ambapo DPP anadaiwa kutofuata kipengele hicho.
Jengo hilo lililokuwa likijengwa mkabala na Msikiti wa Shia Ithnasheri ulioko Barabara ya Indira Gandhi na Kampuni ya ‘Lucky Construction Limited’ ambapo lilianguka majira ya saa 2.30 asubuhi Machi 28, mwaka jana, wakati ujenzi ukiendelea juu huku chini ya jingo hilo shughuli za kibinadamu zikiendelea
Shughuli mbalimbali katikati ya eneo hilo zilisimama kwa siku nzima baada ya jengo hilo kuanguka na kusababisha vifo vya watu (27), na wengine kuokolewa
CHANZO: JMF
No comments:
Post a Comment