Thursday, 6 March 2014

LUPITA NDANI YA POZI NA RHIHANNA....

Mshindi wa tuzo ya Oscar, Lupita Nyong’o, Jana (March 5) alihudhuria kwenye maonesho ya mitindo ya wiki yaliyofanyika Paris inayojulikana kama ‘Miu Miu Fashion Show’, ambapo mastaa wengi walihudhuria ikiwa ni pamoja na Rihanna.
Rihanna alikutana na Lupita Nyong’o ambapo walikaa pamoja na kupiga picha kadhaa ambazo zilipostiwa na Lupita Nyong’o.  
Kwa mujibu wa ripoti, wawili hao ndio waling’ara zaidi kimavazi katika show hiyo, huku Lupita akionekana kuwa mchangamfu na kuzitumia dakika 40 za mwanzo zilizoongezwa kwa ajili ya kumsubiri Rihanna kujitambulisha vizuri kwa wageni wengine waliokuwa wamekaa nae kwenye viti vya mbele.
Baada ya picha hiyo, wengi walianza kutoa maoni yao kwenye mitandao wakidai wanatamani kumuona Lupita Nyong’o kwenye video moja ya wimbo wa Rihanna.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!