BABA wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba anaonekana kuendelea kuwewesekea mali za mwanaye baada ya kuibuka na kudai kuwa, atampeleka Segerea (jela) mzazi mwenzake, Flora Mtegoa kwa madai kuwa amezifuja mali za marehemu.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni kwa njia ya simu, baba Kanumba alisema, ameona taarifa kwenye gazeti kuwa mali nyingi za marehemu Kanumba zimeuzwa huku yeye akiwa hajaambulia chochote.
“Huyu mama Kanumba ana laana yangu, amefuja mali za mwanangu kwa kushirikiana na Seth, mimi sijashirikishwa, nisipopata chochote tutafikishana pabaya,” alisema mzee huyo.
Kuhusiana na hilo, mama Kanumba huyu hapa: “Kwa mila za Kisukuma Kanumba siyo mwanaye kwa kuwa hajanioa, hivyo kuhusu suala la mali kama anazijua zinazomhusu aonyeshe moja baada ya nyingine hapo itakuwa sawa.
CRD: GPL
No comments:
Post a Comment