Wednesday 11 December 2013

WANAOSAJILI SIMU KWA MAJINA BANDIA KUKIONA






Serkali imewaonya kuwa itawachukulia hatua watu wanaosajili namba za simu kwa kutumia majina kwa kuwafunga miezi sita jela au kutozwa faini.

Onyo hilo lilitolewa Bungeni na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema, aliyetaka watu wenye tabia hiyo kwa lengo la kufanya uhalifu, kutuma ujumbe wa matusi na mengineyo watachukuliwa hatua gani.

Profesa Mbarawa alisema suala la usajili wa namba za simu ni la kisheria na linaendelea vizuri lakini kwa yeyote anayesajili simu kwa majina bandia, akibainika watachukuliwa hatua za kisheria.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!