Wednesday 11 December 2013

WANANCHI KUTOA HESHIMA ZAO ZA MWISHO KWA MAREHEMU NELSON MANDELA


Mwili wa hayati Nelson Mandela umewekwa katika jengo la kitaifa la Union ambako aliapishwa wakati aliingia mamlakani mwaka 1994 ili wageni waweze kuutizama.






Mwili wa Mandela ukisindikizwa na polisi Afrika Kusini.

Jeneza lake likiwa limefunikwa bendera ya taifa , lilipitishwa kwa umma likisindikizwa na msafara wa magari na pikipiki.
Wanajeshi waliobeba jeneza hilo walisonga hatua kwa hatua hadi katika Majengo ya union eneo alikoapishwa kuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika kusini 1994.
Mwili huo sasa utaweza kutizamwana wageni mashuhuri pamoja na wananchi wa kawaida.
Wageni hata hivyo hawaruhusiwa kupiga picha.
Mwili wa Mandela utawekw akatika hali hiyo kwa siku tatu zijazo hadi atakapozikwa Jumapili.
Leo jioni wasanii mbali mbali wa Afrika Kusini watashiriki katika tamasha maalum la kumuenzi Mandela na ambalo wananchji wataruhusiwa kuhudhuria bila malipo.
SOURCE. BBC SWAHILI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!