Wednesday, 4 December 2013

WAKUU TAASISI ZA USALAMA NCHINI WAZUIWA KUSTAAFU



RAIS Jakaya Kikwete amewaongezea muda wa miaka miwili, wakuu wote wa Idara za Ulinzi na Usalama nchini, RAI Jumatano lina habari kamili. Taarifa za uhakika zimeeleza kuwa wakuu walioongezewa muda ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema, Mkuu wa Majeshi Jenerali, Davis Mwamunyange, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Rashid Othman na Naibu Mkurugenzi wa Idara hiyo, Jack Zoka.

Kwa mujibu wa taarifa za ajira za wakuu wa usalama nchini, idadi kubwa ya wakuu hao walikuwa wamalize utumishi wao kwa mujibu wa sheria mwishoni mwa mwezi huu. Mmoja wa wakuu wa idara hizo nyeti aliyekuwa astaafu mwishoni mwa mwezi huu ni IGP Mwema, ambaye awali alishamaliza muda wake, lakini aliombwa kuendelea kushikilia nafasi hiyo kwa miezi sita zaidi.

Imeelezwa kuwa IGP Mwema alikataa kuongezewa muda wa zaidi, lakini aliombwa kukubali na kuwa tayari kuongezewa miezi sita, ambayo ilikuwa inafikia kilele Desemba 30, mwaka huu.



No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!