Monday, 9 December 2013
TABU LEY AZIKWA KINSHASA
Shughuli ya mazishi ya marehemu Tabu Ley Rochereau gwiji wa Rumba Afrika, inaendelea mjini Kinshasa, DRC leo. Viongozi wa serikali ya DRC wamehudhuria mazishi hayo huku waakilishi kutoka nchi jirani ya Congo Brazaville pia wamehudhuria mazishi hayo.
Tabu Ley alifariki mwezi Novemba akiwa na umri wa miaka 76 akipokea matibabu nchini Ubelgiji. Wengi walimkumbuka Tabu Ley kwa mziki wake na kwa talanta yake kwa utunzi wa nyimbo zake zilizowagusa watu wengi Afrika. Tabu Ley amefanyiwa mazishi ya kitaifa
Baadhi ya nyimbo alizoimba zilikuwa Adios Thethe na Mokolo nakokufa, na zilisaidia katika kufanya mziki wa Rumba kupendwa sana.
Alikimbilia usalama wake wakati wa utawala wa aliyekuwa Rais Mobutu Sese Seko kati ya mwaka 1965 na 1997, na mnamo mwaka 1990, Serikali ya Mobutu ikapiga marufu album yake Trop, c'est trop.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment