Monday 9 December 2013

RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA YA WATANZANIA KATIKA SHEREHE YA YA MIAKA 52 YA UHURU.





Rais Jakaya Kikwete ameongoza mamia ya Watanzania katika sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika na kuwataka kuyaenzi na kuyazingatia yale yote yaliyoiwezesha Tanzania kupiga hatua za maendeleo ya kiuchumi katika nyanja zote.
Katika sherehe hizo zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, rais Daktari Jakaya Kikwete ameingia uwanjani hapo akiwa katika gari la wazi akiwa ameambatana na mkuu wa majeshi Janerali Davis Mwamunyange na kuzunguka uwanja wa Uhuru akipungia mkono mamia ya Watanzania waliofurika uwanjani hapo, kisha kupanda katika jukwaa maalum ambapo mizinga 21 ilipigwa na hatimaye alikagua gwaride la vikosi vyote vya ulinzi na usalama.
Akihutubia mimia ya wananchi waliofurika uwanjani hapo,rais Kikwete amewataka Watanzania kuyaenzi mafanikio hayo yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 52 ya Uhuru ili kuwezesha kupatikana mafanikio makubwa zaidi katika kipindi cha miaka 52 ijayo.
 aidha akizungumzia kifo cha rais mstaafu wa Afrika kusini Nelson Mandela ,rais Kikwete amahasa Watanzania kujifunza kusamehe kama alivyokuwa rais Nelson Mandela badala ya kuwaza kulipa kisasi na kusisitiza Nelson Mandela alikuwa kiongozi wa Afrika ambae katika uhai wake alichukia ukiukwaji wa haki za binadamu na amepigania uhuru wa watu weusi.
 Awali wakizungumza na waandishi wa habari katika sherehe hizo baadhi ya wananchi wameiomba serikali kuweka mkazo zaidi katika ulinzi wa mipaka ya nchi ili kudumisha amani ya nchi huku wengine wakiomba mchakato wa kupata katiba mpya uwe wa usawa na uwazi ili usije kuvuruga amani iliyokuwepo kwa miaka 52 ya uhuru.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!