Saturday, 7 December 2013

MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA HIGH LEVEL GROUP KUHUSU ELIMU NA AFYA KWA VIJANA WA NCHI ZA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini ya Afrika wa UNAIDS na Mwenyekiti wa High Level Group Profesa Sheila Tlou wakati wa ufunguzi wa mkutano wa High Level Group unaofanyika Cape Town nchini Afrika Kusini tarehe 6.12.2013.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa siku mbili wa High Level Group, unaofanyika huko Cape Town tarehe 6 na 7, Desemba 2013. Mkutano huo unazungumzia masuala ya elimu na afya kwa vijana wanaoishi katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na viongozi wengine wa High Level Group wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kanda wa UNAIDS, Profesa Sheila Tlou na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki Mheshimiwa Jesca Eriyo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa siku mbili wa High Level Group, unaofanyika huko Cape Town tarehe 6 na 7, Desemba 2013. Mkutano huo unazungumzia masuala ya elimu na afya kwa vijana wanaoishi katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpongeza kijana Remmy Shawa, mjumbe wa High Level Group mara baada ya kutoa mada yake 'Background to the East and Southern Africa Commitment Process' kwenye mkutano wao wa siku mbili unaofanyika Cape Town nchini Afrika Kusini tarehe 6.12.2013. PICHA NA JOHN LUKUWI

No comments:

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!