Saturday, 7 December 2013

MAHAKAMA KUU UINGEREZA YAITAKA AFRICAN BARRICK GOLD KUZILIPA FIDIA FAMILIA ZA WANAVIJIJI WALIOUAWA TANZANIA



Mahakama Kuu nchini Uingereza imeiamuru Kampuni ya African Barrick Gold (ABG), yenye makao ofisi zake jijini London, kuondoa mahakama kesi iliyoifungua dhidi ya watanzania na kuitaka kuwalipa fidia raia hao.

Hatua hii ni pigo kwa Kampuni hiyo inayoendesha shughuli za uchimbaji wa madini katika wilaya ya Tarime mkoani Mara ambapo ABG ilishitakiwa katika Mahakama hiyo na wanakijiji kumi na wawili wanaoishi jirani na migodi ya Kampuni hiyo kufuatia vifo vya vya jamaa zao sita waliofariki kwa kupigwa risasi na walinzi wa migodi hiyo mwaka 2011.

Katika kesi hiyo, wanakijiji hao, kupitia Kampuni ya Sheria ya Leigh Day, Kampuni ya ABG na kampouni yake dada ijulikanayo kama North Mara Gold Mine Limited (NMGML), walishtakiwa kwa kuhusika moja kwa moja na vifo hivyo. Katika maelezo ya kesi hiyo ilisemekana ndugu sita wa wanakijiji hao waliuliwa ndani ya eneo la mgodi na mwingine amepooza kufuatia mashambulizi hayo ya risasi.

Katika hatua za kuvuruga kesi hiyo iliyokuwa imefunguliwa nchini Uingereza mnamo Machi 28, 2013; mwezi wa Julai Kampuni ya NMGML ilifungua mashtaka dhidi ya wanakijiji hao nchini Tanzania wakiiomba Mahakama kutamka kuwa Kampuni hiyo ilikuwa haihusiki na vifo hivyo.

Hata hivyo mwanasheria wa wananchi hao aliwasilisha mkakati huo wa NMGML kwenye Mahakama ya Kuu ya Uingereza ambao waliiagiza Kampuni hiyo kuondoa mashtaka waliyofungua nchini Tanzania

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!