Wednesday 11 December 2013

KOCHA WA SIMBA ATAKA DK 180 KUIMALIZA YANGA!

Kocha Mkuu wa Simba, Zdravok Logarusic.


Na Khadija Mngwai
KOCHA Mkuu wa Simba, Zdravok Logarusic, amesema anahitaji mechi mbili zaidi zikiwa ni dakika 180 ili kuweza kukipima kikosi chake kabla ya mechi yao ya Mtani Jembe dhidi ya Yanga.
Mechi ya Mtani Jembe inatarajiwa kupigwa Desemba 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Logarusic amepewa mkataba wa miezi sita wa kuitumikia Simba baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Abdallah Kibadeni.
Akizungumza na Championi Jumatano, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, alisema kocha huyo tayari ameshakiona kikosi na kusema kuwa anataka mechi mbili kabla ya kuivaa Yanga.
“Tutacheza na KMKM lakini kocha amehitaji mechi nyingine zaidi ambapo tutacheza mbili kabla ya kuivaa Yanga.
“Lengo la kocha ni kuangalia uwezo wa kila mchezaji ili aweze kuona viwango vyao na kuweza kupanga timu. Tayari ameshawaona kwenye mazoezi na sasa anataka awaone jinsi wanavyocheza kwenye mechi,” alisema Mtawala.
Hii ina maana kuwa, kocha huyo atatumia dakika 180 uwanjani ili kujua ni jinsi gani timu yake inaweza kuisambaratisha Yanga

GPL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!