Wednesday 11 December 2013

BANK OF AFRICA KUONGEZA MATAWI ZAIDI NCHINI


SONY DSCMkurugenzi Mtendaji wa benki ya Afrika, BOA bank,  Ammish Owusu akiongea na waandishi wa habari katika siku ya familia“Family Day”  iliyoshirikisha wafanyakazi wa benki hiyo na familia zao na wadau mbalimbali iliofanyika kwenye fukwe za Hotel ya Landmark Mbezi beach jijini Dar es Salaam.

002Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Afrika, BOA bank Ammish Owusu akiwa amembeba mtoto wa mfanyakazi wa benki hiyo katika siku ya familia iliyoshirikisha wafanyakazi wa benki hiyo.
HABARI PICHA, NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM
Bank of Africa-Tanzania, imetangaza mpango wa kuongeza matawi zaidi nchini ili kufikia matawi 30 ifikapo mwaka 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa bonanza la wafanyakazi na familia zao, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, bwana Ammissh Owusu-Amoah alisema uongezaji huu wa matawi unaenda sambamba na uhitaji wa huduma za kibenki nchini pamoja na kukua kwa uchumi hapa nchini.
‘Kwa sasa tuna jumla ya matawi 19, na tuko kwenye nchi kumi na saba barani Afrika, na lengo letu ni kuhakikisha tunaongeza matawi ili kuhakikisha tunamfikia kila mtanzania’’ alisema Owusu.
Kwa upande mwingine pia bwana Owusu alisistiza kipaumbele cha benki yake katika kuwasaidia wajasiriamali wadogo,kwa kutenga dola za kimarekani milioni kumi na mbili, huku pia kukiwa kukiwa na utaratibu wa kutoa elimu ya ujasiriamali.
Kwa mwaka huu BOA wamefungua matawi kwenye miji ya Mtwara na Kahama ikiwa ni kiashiria cha benki kuwafikia wateja wengi Zaidi hapa nchini.
Akizungumzia bonanza la wafanyakazi, Meneja Masoko wa BOA, bwana Solomon Haule aliema dhumuni kuu la siku hiyo ni kuwapa wafanya kazi na familia zao nafasi ya kupumzika hali ambayo itaongeza ubunifu kazini.
Solomon alisisitiza kuwa familia ni sehemu muhimu kwenye miiko ya benki yao, na BOA itahahkikisha kuwa wafanyakazi wa BOA wanapata fursa ya kukutana mara nyingi ili kujenga ushirikianao Zaidi kati yao ndani nan je ya ofisi.
BOA ina matawi 19 hapa nchini, huku ikiwa iko kwenye nchi kumi na saba barani Africa. Matawi 10 yapo Dar es Salaam, huku mengine 9 yakiwa Arusha, Mwanza, Kilimanjaro (Moshi), Morogoro (Morogoro mjini na Mtibwa), Mbeya, Tunduma Kahama na Mtwara.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!