Wednesday, 13 November 2013

VIONGOZI MBALIMBALI WAHANI MSIBA WA DKT. SENGONDO MVUNGI NYUMBANI KWAKE JIJINI DSM LEO.




Rais Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakimfariji mke wa marehemu Dkt Sengondo Mvungi...
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akitia saini kitabu cha maombelezo ya kifo cha Mjumbe wa Tume hiyo Dkt. Sengondo Mvungi nyumbani kwake Kibamba jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete (katikati) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kushoto) nyumbani kwa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi walipokwenda kuipa pole familia. Kulia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia na Mjumbe wa Tume Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Richard Lyimo akimpa pole mke wa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi, Bi. Anna Mvungi wakati Wajumbe wa Tume walipokwenda kumpa pole.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba wakifurahia jambo na Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe (kushoto), Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Mjumbe wa Tume Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim (kulia) walipokutana nyumbani kwa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi Kibamba jijini Dar es Salaam. (Picha na Tume ya Katiba).

Tume
ya Mabadiliko ya Katiba inawafahamisha wananchi kuwa taratibu za
kuusafirisha mwili wa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyefariki
nchini Afrika Kusini zimekamilika na mwili wake unatarajia kuwasili
nchini siku ya Ijumaa, Novemba 15, 2013.

Baada ya kuwasili, mwili huo utahifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Aidha,
siku ya Jumamosi, Novemba 16, 2013 kutafanyika Ibada ya mazishi katika
Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam kuanzia saa
4:00 asubuhi. Baada ya misa, marehemu ataagwa katika Viwanja vya
Karimjee kuanzia saa 6:30 mchana siku hiyohiyo ya Jumamosi, Novemba 16,
2013.

Aidha,
Marehemu Dkt. Mvungi anatarajiwa kusafirishwa siku ya Jumapili, Novemba
17, 2013 kwenda Kisangara Juu, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro kwa
ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu, Novemba 18,
2013.

Dkt.
Mvungi alifariki jana (Jumanne, Novemba 12, 2013) katika Hospitali ya
Millpark jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini alikopelekwa kwa ajili
ya uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili
(MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya
ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani
usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.

Wakati
huohuo, Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiongozwa na
Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba leo (Jumatano, Novemba 13, 2013)
wameungana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete kufika nyumbani kwa marehemu Dkt. Mvungi eneo la
Kibamba jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa pole kwa familia, ndugu
na jamaa wa marehemu Dkt. Mvungi. CHANZO : 
 Mtaa Kwa Mtaa Blog


WAKATI HUO HUO TAARIFA TULIZOZIPATA ZINASEMA 
kova1
Kamanda wa Kanda Maalum Dsm, Kamishina wa Jeshi la Polisi (ACP) Suleiman Kova.
.Mtuhumiwa huyo ni  wa kumi kukamatwa kuhusiana na tukio hilo
Siku moja baada ya nguli ya sheria za katiba nchini, Dakta Sengodo Mvungi kuaga dunia nchini Afrika Kusini, Jeshi la Polis Kanda Maalum Ds, linamshikilia mtuhumiwa mmoja John Ikondia Mayunga (56) kwa kosa la kushiriki kikamilifu kwenye mauaji ya mwanasheria huyo na mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kanda Maalum Dsm, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Suleiman Kova amesema mtuhumiwa huyo ni mkazi wa kiwalani walipata taarifa kwa raia wema kwamba alishiriki kikamilifu kwenye tukio hilo lilosababisha kifo cha Dakta Sengodo Elibariki Mvungi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!