Wednesday, 13 November 2013

NINI KIFANYIKE KUPUNGUZA AJALI ZA BARABARANI ? HII NI AJALI YA BODABODA HUYU KAKA AMEPOTEZA MGUU ... TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI....


Dereva wa pikipiki ya abiria maarufu kama bodaboda jina halijafahamika mpaka sasa (kwani hawezi kuongea) amepata ajali mbaya na kuvunjika kabisa mguu wake wa kulia mara baada ya kugongwa na lori la mchanga katika eneo la daraja la Mkolani wilayani Nyamagana nje kidogo ya jiji la Mwanza.
Kwa mujibu wa Mwandishi wetu aliyeweza kuwahi kufika ktk eneo la tukio na kutoa msaada wa gari kumfikisha dereva wa pikipiki hiyo aliyopata ajali Hospitali ya Rufaa ya Bugando, annasema kuwa dereva huyo alikuwa akitokea Mkolani kuelekea Buhongwa na Roli hilo lilikuwa likitokea Buhongwa kuelekea Mkolani, imetokea wakati dereva wa roli 'akiovateki' daladala iliyokuwa mbele yake ikibeba abilia, hivyo alipoipita tu daladala hiyo akakutana uso kwa uso na bodaboda.
Baadhi ya bodaboda na wasamalia wema wakimbeba majeruhi kumpeleka kwenye gari la MSD Kanda ya Ziwa ili kumkimbiza hospitali ya Bugando.
Hivi ndivyo mguu ulivyo vunjika baada ya kupata ajali.
Sambamba na kuvunjika mguu pia dereva huyo amevunjika vidole vitatu vya mkono wake wa kulia. 

PICHA KWA HISANI YA PAPARAZI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!