Uchaguzi huo umefanyika licha ya kuwepo wasiwasi kuhusu ukiukwaji wa haki za binaadamu na
vikwazo juu ya uhuru kwenye nchi hizo.
vikwazo juu ya uhuru kwenye nchi hizo.
Mataifa hayo China, Cuba, Urusi na Saudi Arabia, ni miongoni mwa mengine 14 yaliyojishindia viti
hivyo katika uchaguzi wa mwaka, baada ya kupata theluthi moja ya kura za wajumbe wa baraza hilo
lenye makao yake mjini Geneva.
hivyo katika uchaguzi wa mwaka, baada ya kupata theluthi moja ya kura za wajumbe wa baraza hilo
lenye makao yake mjini Geneva.
Nchi nyingine zilizojipatia viti katika baraza hilo lenye wanachama 47, ni pamoja na Algeria, Uingereza
Ufaransa, Mexico, Maldives, Morocco, Namibia, Afrika Kusini, Vietnam na Macedonia.
Ufaransa, Mexico, Maldives, Morocco, Namibia, Afrika Kusini, Vietnam na Macedonia.
Nchi hizo zimechaguliwa jana Jumanne (12.11.2013) na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
lenye wanachama 193, huku balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Samantha Power
akielezea wasiwasi wake kuhusu uteuzi wa baadhi ya nchi.
lenye wanachama 193, huku balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Samantha Power
akielezea wasiwasi wake kuhusu uteuzi wa baadhi ya nchi.
Makundi ya kutetea haki za binaadamu yamepinga uteuzi wa mataifa hayo.
Baraza hilo lakabiliwa na changamoto
Mkurugenzi Mtetezi wa kimataifa wa shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu
la Human Rights Watch, Peggy Hicks, amesema kuwa wanachama hao wanne wapya pamoja na Algeria
walikataa kuwaruhusu wakaguzi wa Umoja wa Mataifa kuzuru kwenye nchi hizo kuchunguza madai
ya kuwepo unyanyasaji na ukiukwaji wa haki.

Hicks amesema wanachama wa baraza hilo itabidi wafanye juhudi zaidi kuhakikisha wanakabiliana
na changamoto kadhaa.
na changamoto kadhaa.
Kwa mujibu wa shirika la utetezi la Umoja wa Mataifa, linaloufuatilia umoja huo, ni nchi nne tu
kati ya wagombea 16 waliokuwa wanawania viti hivyo 14, ndizo zilizokuwa na sifa ya kuwa
wanachama wa baraza hilo la haki za binaadamu. Nchi hizo ni Uingereza, Ufaransa, Macedonia na Mexico.
kati ya wagombea 16 waliokuwa wanawania viti hivyo 14, ndizo zilizokuwa na sifa ya kuwa
wanachama wa baraza hilo la haki za binaadamu. Nchi hizo ni Uingereza, Ufaransa, Macedonia na Mexico.
Mataifa mapya yaliyochaguliwa, yataanza kazi rasmi kuanzia mwaka 2014 hadi 2016. Iran na Syria
zilikuwa zinapanga kuwania nafasi hiyo, lakini zilijiondoa baada ya kukosolewa kutokana na rekodi
yao ya haki za binaadamu.
zilikuwa zinapanga kuwania nafasi hiyo, lakini zilijiondoa baada ya kukosolewa kutokana na rekodi
yao ya haki za binaadamu.
Jordan yajiondoa kuipa nafasi Saudi Arabia
Hadi wiki iliyopita, Jordan ilikuwa inagombea kiti hicho, lakini ikajiondoa ili kuiruhusu
Saudi Arabia igombee bila ya kuwa na mpinzani.
Saudi Arabia igombee bila ya kuwa na mpinzani.
Jordan inataka kuwa mjumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua nafasi iliyoachwa
na Saudi Arabia, ambayo ilikataa kiti hicho kuanzia mwaka 2014 hadi 2015, mwezi uliopita.
na Saudi Arabia, ambayo ilikataa kiti hicho kuanzia mwaka 2014 hadi 2015, mwezi uliopita.
Tangu kuundwa kwake, Baraza la Haki za Binadaamu la Umoja wa Mataifa limekuwa likikabiliwa
na changamoto kadhaa, huku kazi ya kuzifuatilia nchi wanachama ikiwa ni jukumu gumu.
na changamoto kadhaa, huku kazi ya kuzifuatilia nchi wanachama ikiwa ni jukumu gumu.
Aidha, Bibi Power amesema uchaguzi huo unakumbusha kwamba kazi muhimu ya baraza hilo bado
haijakamilika.
haijakamilika.
Nchi zilizoangushwa katika uchaguzi huo ni Uruguay, iliyoshindwa na Cuba na Mexico katika
viti vya Amerika ya Kusini na kundi la Caribbean, pamoja na Sudan Kusini ambayo ilishindwa
kupata kura za kutosha ili kushinda kiti kimoja kati ya vinne vya Afrika
DW. KISWAHILI.
viti vya Amerika ya Kusini na kundi la Caribbean, pamoja na Sudan Kusini ambayo ilishindwa
kupata kura za kutosha ili kushinda kiti kimoja kati ya vinne vya Afrika
DW. KISWAHILI.
No comments:
Post a Comment