Thursday, 12 September 2013

POLISI WASHINDWA KUMPANDISHA SUGU KIZIMBANI KUFUATIA VURUGU ILIYOTOKEA BUNGENI.







WAKATI rufaa ya kupinga ubunge wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) ikitarajiwa kuanza kusikilizwa katika Mahakama ya Rufaa Dodoma, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Wakili wake, Godfrey Wasonga, kimeiomba mahakama hiyo kuifuta kesi hiyo.

Kwa mujibu wa wakili huyo, sababu ya kuomba kufutwa kwa kesi hiyo ni kutokana na walalamikaji wote kujitoa na kuapa mahakamani kuwa hawapo tayari kuendelea na kesi hiyo.

Hata hivyo wakazi wawili wa Kijiji cha Makiungu mkoani Singida, Shabani Selema na Paskali Hallu, ambao walifungua kesi ya msingi kupinga ubunge wa Lissu, tayari walikwisha kuweka bayana kukubaliana na hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma Aprili, mwaka huu.

Mara kadhaa wananchi hao wamenukuliwa wakimlalamikia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kuwa anawashinikiza kuendelea na rufaa hiyo licha ya kwamba walikwisha kujitoa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Wasonga ambaye alikuwa akiwatetea wanachama hao katika kesi hiyo, alisema kuwa baada ya kuwasiliana na wateja wake walimwambia hawapo tayari kuendelea na kesi hiyo.

“Ni kweli walalamikaji wote wamejitoa na mimi kama wakili sioni haja ya kuendelea, nitakuwa namwakilisha nani? Nimeongea nao jana, hakuna mwenye nia ya kuendelea na kesi,” alisema

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!