Mkazi wa Jang’ombe Visiwani
Zanzibar, Pili Hija (24 - pichani), amejifungua watoto walioungana huku mmoja
akiwa hana kichwa. Watoto
hao ambao wapo Wodi namba 36 katika Jengo la Wazazi la Hospitali ya Taifa
Muhimbili mbali na kuzaliwa mmoja akiwa hana kichwa, wameungana sehemu ya uti wa
mgongo, mkono mmoja na wanatumia njia moja ya haja kubwa.
Akizungumza
na mwandishi wetu jana, mama wa watoto hao, alisema: “Nilijifungulia nyumbani,
nilisikia uchungu mara moja na hapo hapo nikajifungua kwa njia ya kawaida na
jirani yangu ndiye aliyenisaidia,”alisema na kuongeza:
“Nilijifungua saa moja
asubuhi, nilijua nitazaa pacha kwa kuwa nilishafanya kipimo katika Hospitali ya
Makunduchi, wakaniambia nitajifungua pacha lakini mmoja si binadamu ni
kiwiliwili.
Daktari wa Upasuaji wa
Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk Zaituni Bokhary alisema; “Hii ni mara ya
kwanza kwa jambo hili kutokea katika miaka ya hivi karibuni. Mara ya mwisho
lilitokea mwaka 1984
WAKATI HUO HUO TAARIFA ZINASEMA, MADAKTARI WAMEFANIKIWA KUWATENGANISHA MIILI YA MAPACHA HAO.
No comments:
Post a Comment