Siku chache baada ya
kuibuliwa kwa kashfa ya kupitishwa kiholela kwa dawa za kulevya katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Jeshi la Polisi limemwondoa Kamanda
wa Polisi wa Viwanja vya Ndege Kamishna Msaidizi (ACP), Deusdedit Kato pamoja na
Mkuu wake wa Upelelezi, David Mwafwimbo.
Mbali
ya maofisa hao, pia jeshi hilo limemwondoa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara,
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Linus Sinzumwa, naye ikiwa ni miezi michache
baada ya kutokea kwa ghasia wakati baadhi ya wakazi wa huko walipokuwa wakipinga
mpango wa Serikali wa ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam.
Nafasi ya Kamanda Sinzumwa
imechukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Zelothe Stephen
kutoka Makao Makuu ya Polisi.
Taarifa iliyotolewa jana na
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso ilisema Mkuu wa jeshi hilo, Inspekta
Jenerali (IGP), Said Mwema amemteua, ACP Selemani Hamisi kuchukua nafasi ya Kato
ambaye anahamishiwa makao makuu ya jeshi hilo. Kabla ya uteuzi huo, Kamanda
Hamisi alikuwa Makao Makuu Idara ya Upelelezi.
No comments:
Post a Comment