Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) (watano kutoka kushoto msitari wa mbele) akiwa anandamana pamoja na waandamanaji wanaopinga ujangili wa tembo ‘Tembea kwa ajili ya Tembo’ mara baada ya kuwapokea leo, Ubungo jijini Dar es Salaam asubuhi. Maandamano hayo yamechukua muda wa siku 19 na waandamanaji wametembea kilomita 650, kutoka Jijini Arusha.
Matembezi hayo ya kupinga ujangili yameandaliwa Bw. Patric Patel, Mkurugenzi, African Wildlife Trust (wanne kutoka kulia msitari wa mbele) yakiwa na lengo la kuelimisha wananchi na Ulimwengu mzima kwa ujumla juu ya madhara ya ujangili. Matembezi yamehusisha raia wa nchi mbalimbali duniani.
Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) ambaye ndiye mgeni rasmi katika kilele cha matembezi hayo ametoa wito kwa wananchi wote waendelee kushirikiana na serikali kupiga vita ujangili kwa kuwafichua majangili popote wanapowaona; na taasisi zote za umma zishirikiane kupambana na ujangili ili kuutokomeza kabisa.
No comments:
Post a Comment