Pages

Monday, 23 September 2013

KOCHA WA TIMU YA SUNDERLAND UINGEREZA PAOLO DI CANIO AFUNGASHIWA VIRAGO BAADA YA TIMU HIYO KUSHIKA MKIA KATIKA LIGI MASHUGHURI DUNIAN



Paolo Di Canio sacked by Sunderland



kocha wa timu ya Sunderland inayoshiriki Ligi kuu ya uingereza  Paolo DI Canio muda si mrefu amefungashwa virago na uongozi wa Sunderland baada ya michezo mitano na timu hiyo kushika mkia kwenye ligi hii mashuhuri duniani.
 
Juzi Jumamosi Sunderland wakiwa uwanjani kwao walicharazwa bao 3-0 na timu ya West Bromwich Albion.
Baada ya kula kichapo hicho Di Canio aliwasema wachezaji wake "The players have rubbish in their brains" kuwa vichwa vyao vina takataka.
 
Itakumbukwa kuwa Di Canio alipopewa timu ya Sunderland kulitokea mkwaruzano mkubwa na baadhi ya vigogo wa Sunderland hali iliyopelekea Aliyekuwa waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza chini ya utawala wa chama cha Labour Bwana David Miliband kujiuzulu kwenye uongozi wa timu ya Sunderland sababu kubwa ikiwa ni kuteuliwa Di Canio.
 
wako makocha wengi wanatajwa kuchukua mikoba ya Di Canio kwenye timu ya  Sunderland lakini Roberto DI Mateo aliyekuwa Chelsea ndiye anatajwa sana.

No comments:

Post a Comment