Thursday, 5 September 2013

AGNES MASOGANGE AWATAJA WALIOMTUMA UNGA SOUTH, MTOTO WA KIGOGO NA MFANYABIASHARA



IMEVUJA! Staa muuza nyago kwenye video za wasanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu za Kibongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ na shosti wake, Mellisa Edward kabla ya kupandishwa kizimbani kwa msala wa dawa za kulevya ‘unga’ Afrika Kusini waliingizwa kwenye chumba cha mateso kwa saa 24 ili kutaja waliowatuma.
Habari kutoka kwa chanzo chetu kilichopo jijini Johannesburg nchini humo zilidai kuwa baada ya kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, walipelekwa polisi ambapo walichukuliwa maelezo.
Ilielezwa kuwa mwanzoni waligoma kueleza mzigo huo wa kilo 150 wa unga ulikuwa wa nani hivyo ikabidi polisi wa upelelezi watafute njia nyingine ya kuwalainisha kwa kuwabembeleza kuwa wakieleza ukweli wataachiwa.
MATESO SAA 24
Chanzo hicho kilisema kuwa baada ya mbinu hiyo kushindikana ndipo wawili hao wakaingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ikiaminika kuwa watasema aliyewatuma.
USHUHUDA
“Unajua Sauzi (Afrika Kusini) huwa hawana utani na ishu za madawa ya kulevya. Jamaa (polisi) wana kila aina ya mbinu ya kumfanya mtu aeleze ukweli.
“Katika kutesa unaweza kuingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ambayo nayo huwa yana steji zake.
“Kwanza utaanzia kwenye chumba kilichojazwa siafu wakubwa na huko unaweza usijue kuwa kuna siafu zaidi ya kuona kitu kama red carpet (zuria jekundu) kuanzia sakafuni, ukutani hadi kwenye dari, kumbe wale wote ni siafu.
“Wakishakuingiza mle ndipo utashangaa wale siafu wanacharuka na kuanza kukung’ata mwili mzima, zoezi hilo hufanyika kwa saa 24. Lazima useme ukweli.
“Kama bado ukijifanya mbishi au nunda ndipo unapelekwa hatua nyingine ya kulazimishwa kujisaidia haja ndogo kwenye waya wa umeme.
“Si unajua tena waya wenye umeme na maji vikikutana nini kinatokea? Lazima itatokea shoti ya kutisha kwani ule waya hufuata sehemu yale maji yanapotokea

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!