RAIS MSTAAFU WA MAREKANI BILL CLINTON ATEMBELEA TANZANIA.
Rais wa Mstaafu wa Marekani, Bill
Clinton jana alifanya ziara katika makazi ya watu duni eneo la
Vingunguti, wilayani Ilala Dar es Salaam, ambapo alikagua miradi
midogomidogo ya wananchi inayofadhiliwa na mfuko wake (Bill Clinton
Foundation).Clinton alitembelea eneo hilo akitokea
moja kwa moja Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es
Salaam (JNIA), alipowasili akiwa katika ziara ya nchi mbalimbali za
Afrika kukagua miradi inayoendeshwa na mfuko wake.Katika eneo hilo rais huyo mstaafu
alipokewa kwa shamrashamra mbalimbali ikiwamo ngoma za kiasili huku
baadhi ya wananchi wakipigwa butwaa na kutoamini macho yao kwa kiongozi
huyo kutembelea makazi yao. Aidha, Clinton alipata wasaa wa
kusalimiana na wakazi wa Vingunguti wakiwamo watoto ambao walishindwa
kuzuia hisia zao wakijaribu kumsogelea, hali iliyomsukuma Clinton
No comments:
Post a Comment