MAANDAMANO ya amani
yaliyokuwa yameandaliwa na chama cha demokrasia na maendeleo(chadema) yamegeuka
shubiri kwa wakazi wa jiji la Mwanza baada ya kuibuka mapambano makali baina ya
waandamanaji hao na jeshi la polisi mkoani Mwanza na kusababisha polisi kutumia
nguvu kuwatawanya wafuasi wa chama hicho.
Maandamano hayo ya amani
ambayo yalianzia katika eneo la Buzuruga nje kidogo ya jiji la Mwanza yalikuw
ayakiongozwa na wabunge Highness Kiwia wa Ilemela pamoja na Ezekiel
Wenje kuelekea katika viwanja vya Furahisha yalilenga kumshinikiza Mkuu wa Mkoa
wa Mwanza Ernest Ndikilo kutoa barua zinazodaiwa kuandikwa na ofisi ya Waziri
Mkuu Tamisemi kuwarejesha madiwani watatu waliotimuliwa katika Manispaa ya
Ilemela kutokana na kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo.
Polisi wenye silaha
pamoja na askari kanzu walianza kutanda katika eneo hilo la Furahisha
wakiongozwa na Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Mwanza RCO Konyo
ambaye alikuwa akitumia gari lenye namba za usajili DK 068EXV aina ya Toyota
Land Cruiser
Maandamano hayo ambayo
awali yalionekana kana kwamba yangelimalizika salama yaliwasili katika viwanja
vya Furahisha majira ya saa 5.38 huku yakiongozwa na gari la polisi lenye namba
za usajili za nchi ya Uganda 779 UAG likiwa nimesheheni polisi wenye
silaha nzito ikiwa ni pamoja na mabomu ya machozi na bunduki pamoja na askari
kadhaa ambao walikuwa katikati ya maandamano hayo.
Baada ya maandamano hayo
kuwasili katika viwanja vya Furahisha kwa amani,waandamani hao ambao walikuwa
na mabango mbalimbali yaliyosomeka kuwa ‘Matata hatutaki uendelee kuwa Meya wa
Ilemela rudia kazi yako ya awali, na jingine Jaji Sumari tumechoka kuahirisha
mara kw amara kesi dhidi ya Matata na jingine lililosomeka kuwa RD
Ndikilo tunahitaji barua za kurejeshwa kwa madiwani wetu.
Hata hivyo tofauti na
ilivyokuwa imetangazwa kuwa maandamano hayo ya amani yangelipokelewa na Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo,hakukuwa na kiongozi yoyote wa Serikali ambaye
alikuwepo uwanjani hapo kupokea maandamano hayo.
Kufuatia kutoonekana kwa
kiongozi yoyote wa Serikali,viongozi wa chadema pamoja na wabunge wao
walikutana kwa faragha kwa dakika kadhaa kwa ajili ya kujua hatima ya
maandamano hayo ambapo Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje alipanda jukwaani saa
6.45 na kuwaeleza maelfu ya waandamanaji kuwa wameamua kumtuma Mbunge wa
Ilemela Highnes Kiwia kwenda ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuchukua majibu
kwa ajili ya kuwaletea wananchi walioandamana juu ya hatima ya madiwani hao.
Hata hivyo saa moja
baadae Mbunge huyo alisimama jukwani na wakuwaeleza waandamani hao kuwa simu ya
Mbunge Kiwia ilikuwa haipatikani hivyo kuwataka kuandamana kwenda kwa Mkuu wa
mkoa wa Mwanza kujua kulikoni na hapo ndipo hali ya hewa ilipochafuka.
Akizungumza kwa simu juu ya kutokea kwa vurugu zilizosababisha kupigw akwa mabomu ya machozi,Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu alisema kuwa polisi walifanikiwa kudhibiti vurugu hizo na hadi sasa hawezi kusema ni wananchi wangapi ambao walikamatwa kuhusu vurugu hizo.
No comments:
Post a Comment