Thursday, 1 August 2013

NDUGU ZANGU WATANZANIA TUMSAIDIE HUYU MTOTO AKATIBIWE... KUTOA NI MOYO HATA KIDOGO ULICHONACHO

Mtoto Ashura Mustapha anayesumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi.
Na Martha Mboma

MTOTO Ashura Mustapha (7) mkazi wa Mwandege, wilayani  Mkuranga, Pwani anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi tangu akiwa na mwaka mmoja.…
Akizungumza na mwandishi baba mzazi wa mtoto huyu, Bw Mustapha Makombe,alisema" Mwanangu anateseka sana  jamani ugonjwa huu ulianza kama malengelenge akiwa na mwaka mmoja tukawa tunakwenda Hospitali ndogondogo, lakini baadae tukaamua kumpeleka Muhimbili ambako tulipewa barua ya kuelekeza CCBRT ambako kule ndio wakagundua kuwa mwanangu ana kansa ya ngozi steji ya nne.
"Baada ya kuhangaika katika hospitali nyingi bila mafanikio nikaamua kwenda hospitali ya Regency(Dar) kuomba msaada wa kwenda kutibiwa India.
"pale waliniambia nichange shilingi millioni moja na laki tano kwa ajili ya  tiketi na Viza, ili mwanangu akatibiwe India, hizo hela mimi sina.
"Naomba Watanzania mnisaidie hata kwa fedha za mitandao kwa namba hii 0769 517765, au 071542 4607 ili niweze kumpeleka mwanangu India akatibiwe" alisema baba mzazi wa mtoto huyo.
GPL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!