Monday, 5 August 2013

MTU MMOJA ANAYESADIKIWA KUWA NI JAMBAZI ANUSURIKA KUUAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI.


Jambazi akiwa hoi katika hospitali ya Mwananyamala baada ya kupewa kichapo na wananchi wenye hasira kali.

 
KIJANA mmoja ambaye hajafahamika jina lake anayedaiwa kuwa ni jambazi amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali eneo la Kimara jijini Dar es Salaam. Kijana huyo akiwa na wenzake wawili waliokuwa na silaha za moto tayari kwa kwenda kufanya uhalifu lakini kabla mpango wao haujakamilika polisi waliingilia kati.

Haikuwa kazi rahisi kuweza kumkamata jambazi huyo kutokana na majibizano ya risasi kati yao na polisi. Hata hivyo mmoja wao (pichani juu) alitiwa nguvuni wakati wenzake wawili wakitokomea.
(Picha na Khatimu Naheka / GP

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!